Alhamisi 19 Juni 2025 - 00:44
Wanafunzi wa kike waupongeza ushujaa wa Bibi Imami, mtangazaji wa Shirika la Habari

Hawza/ Sisi, wanafunzi wa kike wa hawza, tunatoa pongezi zetu kwa Bibi Ilham Imami, mtangazaji jasiri wa Shirika la Habari, ambaye aliweza kuuonesha ulimwengu, wanawake na wapenda uhuru wote duniani, somo la hamasa na kusimama imara alilolijifunza kutoka kwa Bibi Zaynab (sa).

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia hatua ya kishujaa ya mtangazaji huyo wa kike wa Shirika la Habari, aliyekuwa hewani moja kwa moja wakati wa shambulio la kinyama la utawala wa Kizayuni dhidi ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, taarifa rasmi imetolewa.

Matini kamili ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim

Katika siku hizi ambapo harufu ya damu ya mashahidi imejaa katika anga ya ulimwengu wa Kiislamu, na mbingu za nyoyo zetu zimejaa machozi kwa sababu ya kuondokewa na makamanda wetu na watu wetu wanyonge, ujasiri wa mtangazaji mwanamke jasiri wa Kiirani wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeonesha kwamba, licha ya hali kuwa ngumu kiasi gani, katu hayawezi kupunguza hata kidogo ujasiri na hamasa ya mwanamume na mwanamke wa Kiirani.

Leo, dada zetu wanajifaharisha zaidi ya wakati mwingine wowote, kuwa warithi wa ujumbe wa Fatima Zahra (as) na khutuba za Zaynab Kubra (as); wanawake ambao hawakuishia tu katika kusubiri, bali walikuwa wenye kuelimisha na kufumbua macho ya jamii; hawakuishia tu kwenye kulia, bali waliendeleza harakati ya mapambano. Mwanamke jasiri wa Iran, kwa kusimama kwake imara, ameuthibitishia ulimwengu mzima kuwa utawala wa jinai wa Kizayuni haufungwi na sheria yoyote ya kimataifa wala ya kibinadamu, na uko tayari hata kuikata sauti ya haki kwa kuushambulia mtandao wa redio na televisheni.

Sisi, mabinti wa Iran ya Kiislamu, mbele ya damu ya mashahidi wetu, mbele ya machozi ya mama waliowapoteza watoto wao, na mbele ya matumaini ya nyoyo za wanyonge wa Palestina, hatutakaa kimya. Utawala huu muovu unaoua watoto hauwezi, kwa shambulizi la kinyonge, kulinyamazisha sauti ya ukweli.

Sisi, wanafunzi wa kike wa hawza, tunatoa pongezi zetu kwa Bi Ilham Imami, mtangazaji jasiri wa Shirika la Habari, ambaye aliweza kuuonesha ulimwengu, wanawake, na wapenda uhuru wote duniani, somo la hamasa na kusimama imara alilolijifunza kutoka kwa Bibi Zaynab (as), na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amzidishie umri na amfanikishe zaidi katika jitihada zake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha